MOROGORO KUJA NA MKAKATI WA KUKUZA PAMBA NA KOROSH
Mkuu wa mkoa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema serikali ya mkoa huo inakusudia kuanza kuhamasisha kilimo cha zao la korosho pamoja na zao la pamba hasa kwa wananchi ili kuimarisha uchumi pamoja na kuongeza pato katika mkoa.
Akitembelea maonesho ya 30 ya nanenane kanda ya mashariki amesema lengo la Mkoa wa Morogoro ni kutaka kuzalisha tani 20,000 hadi 30,000 ifikapo mwakani.
Kaimu meneja bodi ya korosho tawi la Morogoro Jafari Matata amesema, bado hamasa kwa wakulima ni ndogo hasa kwa zao la korosho hivyo bodi hiyo imeandaa mkakati wa kusogeza huduma ya ugani kwa wakulima hao.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ununuzi wa pamba Vitus Lipagila amesema, tayari wameanza mikakati ya kutengeneza mikataba kati yao na wakulima .