Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura akiwa na ujumbe wa maofisa watano kutoka Jeshi la Polisi Tanzania leo jumatatu wameanza rasmi ziara ya kikazi Nchini Ireland ambapo ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Ireland “An Garda Síochána” na kukutana na Deputy Commissioner Anne Marie McMahon.
Maofisa hao wa jeshi Wameweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kubaini, kuzuia na kutanzua makosa ya jinai hususani Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya watoto.
Pia walipata fursa ya kujadili namna ya kushirikiana kwenye eneo la mafunzo kwa maafisa na askari kati ya Jeshi la Polisi Ireland na Jeshi la Polisi Tanzania.