Home KITAIFA MKURUGENZI MTWARA DC ATETA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI

MKURUGENZI MTWARA DC ATETA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Tatu Saidi lssike amefanya mkutano na baadhi ya watumishi zaidi ya 100 wa kada mbalimbali kutokea Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ili kujua kero mbalimbali zinazo wakabili watumishi hao na kuzifanyia kazi.

lssike amesema ziara yake imekua na manufaa makubwa kwa kuwa watumishi wamejitokeza kwa wingi na kutoa kero zao na amewaomba watumishi katika Halmashauri hiyo kuwa na ushirikiano.

“Malalamiko yao wengi ni upande wa malipo,malipo yanachelewa,malipo ya uhamisho,likizo na staili mbalimbali za kiutumishi ukiwa mbali hawawezi kuelewa kwanini yana chelewa ila ukikutana nao unawalekeza pengine ni bajeti wanaweza kuelewa.”

“Kipaumbele chetu kikubwa kabisa ni makusanyo,kuzingatia 10% tunaipata kutokana na mapato yetu,kipaumbele cha kupunguza hoja pamoja na huduma bora kwa wananchi na ili wananchi wapate huduma bora lazima tuwasikilize watumishi kwasababu ndio wanaotoa huduma.”Amesema Issike.

Kwa upande wao watumishi wamempongeza Mkurugenzi huyo kwa hatua madhubuti ya kuwakutanisha na kusikiliza kero za watumishi hao.

“Haijawahi kutokea mimi nimeanza kazi mwaka 1991 katika Halmashauri hii na huyu ni Mkurugenzi wa kwanza kukutana na watumishi ili kusikiliza kero zao tunaahidi kumpa ushirikiano kwasababu sisi ni watekelezaji wa kazi.”Amesema Ali Bango Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilombelo

Kikao hicho cha Mkurugenzi na watumishi wa kada mbalimbali kimefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Madimba.

Previous articleBAYERN MUNICH WANAJIPANGA KUVUNJA REKODI KWA HARRY KANE
Next articleWALIOVAMIA KIA KULIPWA FIDIA KUANZIA MWEZI HUU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here