HAYDOM-MBULU
Mkataba wa Mradi wa ujenzi wa barabara ya Labay-Haydom Km 25 umesainiwa rasmi jana, ikiwa na hatua muhimu ya kuelekea kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo muhimu kijamii na kiuchumi kwa Wananchi wa Wilaya ya Mbulu.
Zoezi la kusaini Mkataba huo, limefanyika jana Mei 19/2023 katika Uwanjwa wa Haydom wilayani Mbulu na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi Injinia Godfrey Kasekenya, Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na wananchi wakiongozwa na Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara Komred Charles Makongoro Nyerere.
Ujenzi wa barabara hii ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, na Dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha Miundombinu ikiwa ni Njia ya Kuchochea Shughuli za Kiuchumi na Kurahisisha Huduma kwa Wananchi.
Akizungumza kwa Niaba ya Wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Mbunge wa Jimbo hilo Komred Flatei Massay amempongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa uamuzi huo muhimu kwa faida ya wananchi wa Mbulu,na ameiomba Serikali isimamie mradi huo kwa ukaribu ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango.