Home KITAIFA MKATABA USIO NA KIKOMO NDIYO MZURI UNAVUNJIKA MUDA WOWOTE

MKATABA USIO NA KIKOMO NDIYO MZURI UNAVUNJIKA MUDA WOWOTE

Na Dishon Linus

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msavatavangu katika kuendelea kuunga mkono uwekezaji unaofanywa na serikali chini ya Dkt. Samia suluhu Hassan, ametoa ufafanuzi wa mkataba wa bandari wakati akiongea na wanachama wa CCM wilaya ya Iringa.

Katika maongezi yake Msavatavangu amesema mkataba unafaida kubwa sana kwani hata mapato yataongezeka ili tuendelee kumsumbua Rais kupata fedha za maendeleo katika jimbo letu la Iringa mjini.

Aidha Msavatavangu amesema wanaosema mkataba hauna ukomo kwanza ndio mzuri kwa sababu mda wowote unaweza kuvunjika “Kwa sasa tunaendana na dunia inavyokwenda na mkataba hauna muda yaani kikomo ni kweli lakini mkataba usio na muda unavunjika mda wowote,mtu aisilazimshe tu kusema wa milele pia unaweza kuvunjika muda wowote kwasababu hauna muda”

Katika manspaa ya Iringa Msavatavangu amesema mkataba wa badari ukisainiwa fedha za maendeleo zitaongezeka, na katika mkataba huo amesema faida yake kwa wa Tanzania ni kubwa kama

“Kama tulikuwa tunapata bilioni 1 kwenye makontena kwa wiki sasa tutapata bilioni 100 kwenye makontena kwa wiki fedha hizo zitanisaidia mimi nikienda kuomba kwa mama za maendeleo ya jimbo letu”

Lakini pia amewatoa hofu wanachama hao kuwa hata wanaosema mkataba huu ni wa Tanzania bara peke yake ni waongo “mkataba unasema Tanzania na sio Zanzibar wala bara peke yake mkataba ni wa Tanzania ambayo inajumuisha nchi zote mbili”.

Akimalizia Msavatavangu amesema “Mimi niwaombe ndugu zangu sisi kama Iringa mkataba huu tuupigie debe kwa kishindo utapunguza bei ya mbolea,vipodozi utapunguza na ugumu wa maisha pia”.

Previous articleCHADEMA YATAKA MKATABA BANDARI USITISHWE, SUGU ALIA NA WIZI SERIKALINI
Next articleFEDHA ZA UJENZI WA ZAHANATI ZASHTUKIWA KUTAFUNWA NA VIONGOZI WA KITONGOJI, MBUNGE AFICHUA MADUDU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here