Msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mjamzito mkazi wa Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu mara tano sehemu mbalimbali za mwili wake na mzazi mwenzake
Msichana huyo ambaye alilazwa katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Dumila iliyopo Wilaya ya kilosa amesema majira ya saa saba usiku wakati akirudi kutoka kwenye sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake alivamiwa na mwanaume aliyezaa nae Mtoto mmoja kisha kupakiwa kwenye pikipiki kwa nguvu na kuondoka naye ndipo akamjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo tumboni,kichwani,mgongoni na kisu kuvunjikia kwenye paja,huku kisa kikitajwa ni kukataa kwenda kulala pamoja wakati tayari wameachana zaidi ya miezi mitatu.
Mganga mfawidhi hospitali ya Mtakatifu Joseph Dkt.Manyele Jacob,alipotibiwa majeruhi huyo amesema baada ya kufikishwa hospitali msichana huyo walimfanyia vipimo vya utra sound tumboni ili kuona amepata madhara kiasi gani lakini walibaini kisu alichochonwa tumboni hakikufika kwenye utumbo lakini alibainika ni mjamzito.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro zinaendelea ili kufahamu ni hatua gani zitachukuliwa kutokana na tukio hilo.