Home KITAIFA MISHAHARA YA APRILI ILIPWE MAPEMA “_ RAIS MWINYI

MISHAHARA YA APRILI ILIPWE MAPEMA “_ RAIS MWINYI

Watumishi wa Serikali Zanzibar wataanza kupokea mishahara yao ya mwezi wa nne kuanzia leo baada ya Rais na Mwenyikiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi kuagiza mishahara hiyo ilipwe.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Charles Hilaly ya Aprili 16, 2023, Rais Mwinyi ameelekeza kufanyika mapema malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa Serikali kwa ajili ya matayarisho ya Sikukuu ya Eid El Fitr.

 

Sherehe hizo zinatarajiwa kuangukia kati ya Ijumaa au Jumamosi ya Aprili 21 au 22, 2023 na Rais Mwinyi anataka wafanyakazi Serikalini kuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi ya sherehe za Eid El Fitr.

 

Previous articleMATAJIRI WAHUSISHWA UFUKUAJI WA MAKABURI MANYONI-SINGIDA_MAGAZETINI LEO JUMATATU APRILI 17/2023
Next articleVIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUSIMAMIA HAKI NA AMANI KWA MANUFAA YA WANANCHI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here