Home KITAIFA MIL.18.6 ZATUMIKA KUKARABATI MADUKA YA UWT YALIYOTEKETEA KWA MOTO NJOMBE

MIL.18.6 ZATUMIKA KUKARABATI MADUKA YA UWT YALIYOTEKETEA KWA MOTO NJOMBE

 

Njombe

Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Njombe imesema kiasi cha shilingi Milioni 18.6 kimekusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali na kutumika kwenye ukarabati wa maduka ya jumuiya hiyo yaliyoteketea kwa moto April,1,2023 huku jumuiya ikihusika kuchangia Milioni 15.9.

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT wilaya ya Njombe Betreace Malekela amebainisha hayo wakati wakikabidhi milango kwa wafanyabiashara mara baada ya ukarabati ambapo amesema milango 9 ndio iliyokuwa imeteketea kabisa kwa moto huku wakiahidi kuongeza na kusogeza karibu miundombinu ya maji itakayosaidia kukabiliana na majanga ya moto.

“UWT wilaya ya Njombe tumechangia Milioni 15,900,000 wadau walituchangia shilingi Milioni 2,705,000 na jumla ya ghalama zote ni shilingi Milioni 18,637,500 wito wangu kwa wafanyabiashara tunaomba mdumishe upendo kati yenu na msiweke kisasi,tumefika hapa kwasababu ya visasi”amesema Betreace Malekela

 

Naye katibu wa UWT wilaya ya Njombe Sauda Mohamed amewaomba wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati pamoja na kuongeza usafi wa maeneo yao ya biashara hali ambayo itaongeza thamani ya biashara zao.

 

Baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Aloyce Chaula na Elizabeth Mpogolo waliopatwa na changamoto hiyo ya moto kwenye maduka yao wamewashukuru wafanyabiashara wenzao kwa msaada walioutoa kwao wakati wa janga hilo huku pia wakiipongeza UWT kwa kukarabati milango kwa wakati na kuwakabidhi ili waendelee na biashara.

Previous articleWANAWAKE NCHINI WATAKIWA KUSHIKAMANA NA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA ZA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI
Next articleSERIKALI YATIA SAINI MRADI WA B.800 UENDELEZWAJI JIJI LA DAR ES SALAM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here