Home KITAIFA MIKATABA YA SEKTA YA UZIDUAJI KUWA WAZI NCHINI

MIKATABA YA SEKTA YA UZIDUAJI KUWA WAZI NCHINI

 

Naibu wa Waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa amesema, Tanzania ni mwanachama wa Asasi ya Kimataifa ya EITI (Extractive Industries Transparency Initiative) na Jukumu lake kuu ni kuhamasisha Serikali kuweka mifumo ya uwazi katika rasilimali madini, mafuta na gesi asilia ili kuboresha mapato na manufaa yanayotokana na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa rasilimali hizo.

 

Katika kutekeleza takwa la uwekaji wazi wa Mikataba Taasisi ya TEITI imeandaa Mpango kazi (Roadmap) kwa ajili ya utekelezaji wa kazi ya uwekaji wazi Mikataba.

 

Amesema,mpango huo umewekwa wazi kwa ajili ya utekelezaji kulingana na matwaka ya kimataifa ya EITI.

Hata hivyo, katika mwaka wa Fedha 2023/24 TEITI imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa mikataba inawekwa wazi ikiwa ni pamoja na kushauriana na Mamlaka nyingine za Serikali namna bora ya kutekeleza takwa hili.

 

Dkt Kiruswa ameyasema leo mapema Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mheshimiwa Jesca David Kishoa mbunge viti maalum kwa niabaya ya Waziri wa Madini Doto Biteko,Mheshimiwa Kishoa alipouliza swali’ ni lini Serikali itaanza kuweka wazi Mikataba ya Sekta ya Uziduaji kama EITI ( The Extractive Industries Transarency Initiative ) Inavyotutaka.

Previous articleDKT. GWAJIMA AONGOZA MENEJIMENTI YA WIZARA KUMUAGA MUWAKILISHI MKAZI WA UNICEF
Next articleMAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here