Home MICHEZO MIGUEL GAMONDI :TUMEJIPANGA KUPAMBANA NA TIMU YEYOTE KLABU BINGWA AFRIKA

MIGUEL GAMONDI :TUMEJIPANGA KUPAMBANA NA TIMU YEYOTE KLABU BINGWA AFRIKA

 

Na Dishon Linus.

Klabu ya Yanga itacheza mchezo wake dhidi ya Al Merreikh ya Sudan na mchezo utachezwa nchini Rwamda kwenye uwanja uliopewa jina la marehemu Pele katika hatua ya pili ya kutafuta nafasi ya kufuzu makundi klabu bingwa Afrika.

Kocha wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema mpinzani wake ndio anakipanga kikosi cha mechi na mpinzani wake ndio anaamua ni mchezaji gani atacheza mechi.

Gamond amesema “Unajua mimi napenda sana kuzifuatilia timu ninazocheza nazo kwa kuzichambua kwa kina na kujua kwenye mechi naingiaje na ndio maana Kuna muda na mimi nabadili kikosi kutokana na namna nilivyomsoma mpinzani wangu na aina ya timu ninayokutana nayo, kikosi changu kinapangwa na mpinzani wangu”- amesema Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi.

Aidha Gamond amesema wamejipanga kupambana na kila mpinzani watakae kutana nae katika hatua zote za klabu bingwa huku malengo yakiwa ni kufuzu makundi ndio kiu yao kubwa.

Previous articleDKT.BITEKO AAGIZA MABADILIKO SHERIA YA MTOTO KUKAMILIKA
Next articleBUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI 3 MWAKA 2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here