Home MICHEZO MIAKA 8 YA HALOTEL “KIVUMBI NA HALOTEL” KAMPENI YAZINDULIWA, GARI ZIRO KILOMITA...

MIAKA 8 YA HALOTEL “KIVUMBI NA HALOTEL” KAMPENI YAZINDULIWA, GARI ZIRO KILOMITA KUSHINDANIWA

 

 

Kampuni ya Mtandao wa mawasiliano ya simu nchini ya Halotel hii leo, Oktoba 30, imezindua kampeni yake mpya ya ‘Kivumbi na Halotel’ ikiwa ni kusherehekea miaka 8 tangu kuanza kutoa huduma za mawasiliano, ambayo imepewa jina la “Kivumbi na Halotel.”

 

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Halotel, Patrick Rwegoshora, ameelezea shauku yake kuhusu sherehe ya miaka 8 na kampeni hii ya “Kivumbi na Halotel,” kwa wateja, akisema, “Halotel, inatambua kwamba mafanikio yake hayawezi kutenganishwa na imani, uaminifu, wa wateja wake kutumia mtandao wao.

 

“Ni kwa shukrani kubwa tunasherehekea miaka 8 ya ufanisi wa mawasiliano nchini Tanzania. Promosheni hii, ya ‘Kivumbi na Halotel,’ ni moja njia yetu ya kusema ‘asante’ kwa wateja wetu kwa kuendelea kuwa nasi. Tunawakaribisha na tutatamani kuona wateja wengi iwezekanavyo wanashiriki na kushinda zawadi za hizi” aliongeza Patrick

Halotel inaadhimisha miaka 8 ya kuwaunganisha watanzania katika huduma za Mawasiliano kuanzia Vijijini mpaka mijini ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa wateja. Promosheni ya “Kivumbi na Halotel,” itakuwa imesheheni zawadi kubwa na ambazo zitaenda sambamba na umuhimu wa miaka nane ya Halotel ikiwa ni ni upekee kama ilivyo safari yenyewe.

 

Katika Kampeni hii Kama sehemu ya sherehe ya miaka 8, wateja wa Halotel wamepewa nafasi ya kushiriki kampeni na kushinda zawadi kemkem jumla ya 1,510, katika kampeni ya “Kivumbi na Halotel.”

 

Halotel itatoa zawadi mbalimbali kila wiki. Zawadi hizo zinajumuisha simu janja ya mkononi aina ya Samsung Galaxy A 34 5G ikiwa pamoja na laini ya Halotel yenye data ya GB 5 bure. Simu janja ya mkononi ya Samsung Galaxy M14 na laini ya Halotel yenye data ya GB10 bure. Routers za Halotel pamoja na laini Halotel yenye data ya GB5 bure ili kuboresha matumizi bora ya mtandao wa intaneti kwa wateja mahali popote na vifurushi vingine vingi vya kufurahia faida zaidi kutoka kwa huduma za Halotel.

 

Zawadi kubwa kuliko na ya kusisimua ni gari jipya aina ya Mazda CX5, ziro Kilomita, moja ya magari yenye mtindo wa kipekee sokoni. Zawadi hii itatolewa mwishoni mwa Promosheni kwa mteja atakaye bahatika kushinda.

 

Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana na inapatikana kwa wateja wote wa Halotel. Ili kushiriki, wateja wanatakiwa kununua vocha ya kukwangua au kwa Halopesa yenye thamani ya TZS 2,000 au zaidi. Au Kujiunga kifurushi cha huduma chenye thamani ya kuanzia TZS 2,000 au zaidi kwa salio la kawaida au kupitia huduma ya Halopesa ya Halotel.

 

Promosheni ya “Kivumbi na Halotel” inalenga na kuzingatia wateja wote wa Halotel walioko nchi nzima. Lengo kuu likiwa ni kutoa shukrani kwa watanzania na wateja wao kwa ujumla kwa kuendelea kuunga mkono na kuchagua mtandao wa Halotel kwa mahitaji yao ya mawasiliano kwa miaka 8 sasa.

 

Halotel kupitia kampeni hiyo imewahimizwa wateja wake kushiriki kikamilifu na kutumia fursa hii adhimu ya kushinda zawadi mbalimbali na huku wakitengeza nafasi ya kushinda zawadi kubwa kuliko ya gari aina ya Mazda 5CX kutoka Halotel kupitia kampeni hii itakayodumu kwa miezi mitatu kuanzia Oktoba 2023, hivyo nafasi za kushinda ni nyingi kwa kushiriki zaidi..

Previous articlePOLISI SONGWE YAKEMEA ULEVI KUEPUKANA NA AJALI
Next articleDC MAGEMBE AAGIZA WAHANDISI HALMASHAURI YA MJI GEITA KUTEMBELEA MIRADI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here