Sakata la mgomo wa wafanyabiashara katika soko la Kimataifa la Kariakoo limetinga bungeni na kuomba muongozo wa Spika
Akitoa muongozo huo, mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga ameomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamisha vikao vya bunge ili kuweza kujadili suala la mgomo kama hati ya dharura.
Akiwasilisha hoja yake Sanga amesema “Nivyozungumza sasa kunachangamoto ambayo imetokea na kusababisha wafanyabiashara kugoma wakigomea vitendo vya kamatakamata za wafanyabiashara, sheria ya kikodi ya EFD”
Amesema kwasababu Kariakoo ndiyo Dubai yetu Tanzania serikali itazidi kukosa mapato kutokana na mgomo huo “nimeona udharura wa jambo hili na haja ya bunge kulijadili ili shughuli za bunge ziahirishwe kwa muda”
Akijibu hoja Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dk Ashantu Kijaji amesema mpaka sasa hivi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam watendaji wa wizara na wafanyabiashara wapo kwenye majadiliano ili kupata muafaka