Home KITAIFA MBUNGE SWALLE ASHAURI KUANZISHWA DAWATI MAALUM LA KUSIKILIZA KERO ZA WAFANYABIASHARA

MBUNGE SWALLE ASHAURI KUANZISHWA DAWATI MAALUM LA KUSIKILIZA KERO ZA WAFANYABIASHARA

 

Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mkoani Njombe Edwirn Swalle ameshauri Wizara ya Kilimo kuanzisha dawati maalum la kusikiliza na kushughulikia kero za wafanyabiashara kutokana na changamoto wanazokutana nazo wanaposafirisha mazao yao hususani magetini.

Swalle ametoa ushauri huo kwa Waziri wa Kilimo Hussen Bashe ambapo pia ameshauri kuajiliwa mfanyakazi maalum wa kupokea kero za Wafanyabiashara kweye Wizara hiyo.

“Nikuombe Mh! Waziri (Bashe) kwasababu Wizara ya Jinsia na Watoto wanalo dawati maalum la kushughulikia maswala ya jinsia, ninakushauri anzisha dawati maalum la wafanyabiashara kwenye wizara hii ili wapate fursa ya kutoa kero zao moja kwa moja kwako Wizarani”Amesema Edwirn Swalle Mbunge

Ameongeza kuwa”Kumekuwa na kero kubwa sana kwa wafanyabiashara,wengi wanasumbuliwa sana na maofisa wa TRA,mageti kama ya Migori,Mikumi kuna usumbufu mkubwa sana kwa wafanyabiashara mpaka wabunge tupige simu ndio watu waachiwe”

Vile vile akitoa mchango wake leo Bungeni ameiomba serikali kuanza ujenzi wa Barabara kutoka Kibena Njombe mpaka Lupembe ikiwa ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema kufufuliwa kwa mashamba ya chai jimboni kwake kunatakiwa kwenda sambamba na kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo muhimu inayo unganisha mkoa wa Njombe na Morogoro.

Previous articleUTAFITI WA KISAYANSI UTUMIKE KATIKA KULETA MAENDELEO NCHINI – DKT. JINGU
Next articleMBUNGE NJEZA AZIDI KUPAMBANIA BARABARA ZA JIMBONI KWAKE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here