Home KITAIFA MBUNGE SEKIBOKO ATAKA WATOTO WALINDWE DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

MBUNGE SEKIBOKO ATAKA WATOTO WALINDWE DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekwa vikiripotiwa kuongezeka siku hadi siku katika baadhi ya maeneo Mbalimbali nchini.

Sekiboko amesema kumekuwa na wimbi la vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watoto kama ubakaji na ulawiti hivyo amewaasa wazazi na Walezi kuwa makini kuhakikisha wanawalinda watoto wasifanyiwe vitendo hivyo kwani vinaathiri afya ya mwili, akili na kumfanya mtoto kukosa ujasiri.

Wito huo ameutoa wakati wa ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa katika wilaya ya Handeni yenye lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

‘Nawaomba sana walindeni watoto maana usalama wa mtoto ni muhimu sana wapeni haki zote za msingi kwani mkiwatendea mema watoto hawa mmemtendea Mungu na atawabariki,mkitaka laana basi watendeeni watoto hawa mabaya amesema” Amesema Mbunge huyo wa Viti Maalum.

Sekiboko amesisitiza kuwa wazazi na walezi ndio muhimili wa familia hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanafatilia mienendo ya watoto wao ikiwemo maendeleo ya shule na nyumbani,nakuongeza kuwa Vitendo vya ukatili vinaweza kuathiri mfumo wa ukuaji na maendeleo ya mtoto kiakili, kimwili na kisaikolojia.

Katika hatua nyingine mbunge huyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo amewataka wazazi na walezi pia kulinda watoto wao katika kutumia mitandao ya kijamii vizuri bila kuvuka Maadili yanayotakiwa katika Jamii.

Kwa upande wao wazazi waliohudhuria ziara hiyo walisema kuwa licha ya kufahamu majuku Yao ya kifamilia lakini wanamshukuru mbunge huyo kwa kuwakumbusha namna ya kuendelea kuwalinda watoto wetu.

Amina Dhahabu mkazi wa Chanika handeni alisema kuwa watoto wengi wamekosa maadili kutokana na wazazi kushindwa kusimamia majukumu ya malezi ya watoto kikamilifu.

 

Previous articleWAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI
Next articleSHERIA YA MADINI SURA NAMBA 123 KUFANYIWA MAREREBISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here