Home KITAIFA MBUNGE NJEZA AZIDI KUPAMBANIA BARABARA ZA JIMBONI KWAKE

MBUNGE NJEZA AZIDI KUPAMBANIA BARABARA ZA JIMBONI KWAKE

Serikali imesema kuwa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mbeya ilikwisha kutoa mapendekezo ya kuipandisha hadhi Barabara ya Mjele Ikukwa hadi Mlima Njiwa Wilayani Chunya kuwa barabara ya Mkoa.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa TAMISEMI Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza alipouliza ni lini Serikali itaipandisha hadhi Barabara ya Mjele Ikukwa hadi Mlima Njiwa kuwa ya Mkoa.

Naibu waziri huyo amesema Serikali ya Mkoa wa Mbeya kupitia kikao chake cha tarehe 09 Januari, 2023 ilipendekeza pia kuipandisha hadhi barabara hiyo.

“Baada ya mapendekezo hayo kuwasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, tarehe 24 Februari, 2023 Kamati ya Kitaifa ya Kupanga
Barabara Katika Hadhi Stahiki (NRCC) ilitembelea barabara zilizoombwa kupandishwa hadhi Mkoani Mbeya ikiwemo barabara ya Mjele – Ikukwa hadi Mlima Njiwa,”alisema Naibu.

Kadhalika alisema kuwa Mapendekezo ya Kamati yamewasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na yanachambuliwa na uchambuzi ukikamilika taarifa itatolewa.

Endapo barabara hiyo itakidhi vigezo vya kupandishwa hadhi, itakuwa barabara ya mkoa na itahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD).

Mbunge Njeza amesema kuwa licha ya Waziri wa Ujenzi kuridhia barabara hiyo ihudumiwe na TANROAD ipo kwenye hali mbaya na ametaka kujua ni lini itaanza Ujenzi na iweze kurekebishwa kuanzia Mjele-ikukwa mpaka Mlima njiwa

Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kuwa baada ya kupandishwa hadhi barabara hiyo TANROAD itaanza utejelezaji kwa bajeti ambayo itaanza mwaka wa fedha 2023/24.

“Kwa sasa wenzetu wa TARURA baada ya Juni watatukabidhi na sisi tutaanza utekelezaji huo kwa bajeti mpya,” amesema Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi.

Kadhalika Mbunge Njeza amesema katika hali hiyo ya barabara ipo barabara ya Haporoto Ilea Ishinda ambayo inahudumia wachimbaji wa migodi ya Ilea na Ishinda ni lini barabara hiyo itapata matengenezo sababu nayo ipo katika hali mbaya?

Naibu Waziri Ndejembi amesema kuwa barabara hiyo ilipokuwa TARURA ilitengewa Shilingi Milioni 500 na Roadbod kwa ajili ya matengenezo yake.

“Sasa baada ya kupandishwa hadhi fedha Ile itahamia kwa wenzetu TANROAD ambapo bado watatelekeza kwenye barabara hii kwa hii Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kuijenga,

“Barabarani ya Haporoto-Ilea-Ishinda barabara hii inaurefu wa kilomita 9 na kweli nikiri kwamba barabara hii hali yake si nzuri sana katika mwaka wa fedha ambao tunauanza mwezi unaofuata huu tayari barabara hii imetengewa shilingi Milioni 400 kwaajili ya kuweza kutengeneza Yale maeneo korofi Kwa kumwaga changarawe na kuhakikisha kwamba inapitika vizuri sababu inapelekea katika eneo ambalo linamachimbo hivyo nimtoe hofu mbunge Njeza muda si mrefu ataona utekelezaji wake,” ameeleza Ndejembi.

Previous articleMBUNGE SWALLE ASHAURI KUANZISHWA DAWATI MAALUM LA KUSIKILIZA KERO ZA WAFANYABIASHARA
Next articleTPA KUJENGA GATI JIPYA NA ONE STOP CENTER MTWARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here