Mbunge wa Manyoni Mashariki Mhe. Dkt Pius Chaya, amehitimisha Ziara yake katika Kata zote 19 za Jimbo huku akitatua kero zinazowakabili Wananchi hao na zingine kupeleka katika mamlaka husika kwaajili ya utekelezaji/ utatuzi.
Amehitimisha ziara hiyo katika kata ya Saranda ambapo amezungumza na wananchi, pamoja na kusikiliza changamoto walizonazo.
Akiwa hapo amekagua ujenzi wa maboma ya shule ya msingi Isanjandugu ambayo wananchi wamewezesha ujenzi wake na Mhe. Chaya ameahidi kutoa Kiasi cha Shilingi Milioni 4 ili kuwezesha Ujenzi wa Madarasa hayo na kutatua changamoto ya watoto kufuata huduma ya Elimu kwa umbali mrefu.
Ziara ya Mbunge Dkt. Chaya imedumu kwa Wiki mbili ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, Elimu, Afya, na Maji, Kutoa Vifaa vya michezo na kusikiliza kero za wananchi wake ambapo alipata wasaa wa kutatua changamoto zinazowakabili huku zingine akiahidi kuzipeleka katika mamlaka husika kwaajili ya itatuzi.