Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti Bw. Tundu Lissu, Jumatano leo Mei 17, 2023 hii mkoani Kigoma, wanatarajiwa kuzindua Operesheni ‘+255 Katiba mpya’ Itakayofanyika nchi nzima ikiwa ni maandalizi kueleka Uchaguzi mkuu wa 2025.
Uzinduzi huo utafanyika kwenye uwanja wa Mwanga mkoani Kigoma na baada ya uzinduzi viongozi watagawanywa kwenye makundi mawili ili kuanza safari ya kuzungumza mkoa mzima wa Kigoma.
“Tumesema bila Katiba mpya hatushiriki uchaguzi lakini haimaamishi tusijiandae na siku zote ukitaka kuhakikisha kushinda uchaguzi lazima ujiandae.Tumeanza kujipanga”-John Mrema, Mkurugenzi wa itifaki na mawasiliano