Home KITAIFA ” MAZOEZI YANASAIDIA AFYA KUEPUKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA”_ DC MVOMERO

” MAZOEZI YANASAIDIA AFYA KUEPUKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA”_ DC MVOMERO

 

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Judith Ngulli ameongoza mazoezi ya pamoja wananchi na watumishi wa Wilaya hiyo.

DC Judith amesema kuwa wamekua na utaratibu wa kufanya mazoezi kila jumamosi ikiwa ni mwendelezo wa maagizo wa viongozi wa kitaifa kutaka watumishi wa serikali kushirikiana na viongozi kufanya mazoezi ya pamoja kila jumamosi ya pili ya mwezi ili kuimarisha afya ya mwili lakini pia kuongeza upendo, umoja,amani na ushirikiano mahali pa kazi.

DC amesema mazoezi yamekua yakiwasaidia katika afya hasa kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza, lakini yamewaweka wananchi, watumishi na viongozi pamoja kila Jumamosi ya pili ya mwezi umekuwa ni utaratibu wa Wilaya ya Mvomero kukutana pamoja kwa watumishi, wananchi na viongozi na kufanya mazoezi ya pamoja ili kuimarisha afya zao.

Anasema ili mtumishi afanye kazi vizuri anahitaji kuwa na afya bora, amani na furaha hivyo kwa kutambua umuhimu wataendelea kufanya hivyo kila inapobidi na jumamosi ya pili ya mwezi watafanya pamoja.

Previous articleRAIS SAMIA AFANYA MAGEUZI MAKUBWA MIRADI YA MAENDELEO BUKOMBE-DKT BITEKO
Next articleWAHITIMU WATAKIWA KUEPUKANA NA VITENDO VYA UTUMIAJI MADAWA YA KULEVYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here