Mtangazaji Maulid Kitenge amesema, kitendo cha watu mbalimbali kupotosha kuhusu ukweli mkataba wa uendeshaji na uendelezaji wa bandari za Tanzania, wamemua kufunga safari hadi Dubai Falme za Kiarabu yalipo makao makuu ya kampuni ya DP WORLD inayotegemea kupewa dhamana ya uendeshaji na uendelezaji wa bandari za Tanzania ili kupata ukweli wa jambo hilo ili kuwaelimisha wananchi ukweli kuhusu mkataba huo.
Kitenge amewatupia lawama baadhi ya Watanzania wanaopotosha ukweli kuhusu mkataba wa ukodishwaji wa bandari za Tanzania huku akisema wengi wao hawaifahamu bandari na hawajawahi hata kutumia huduma za bandari.
“kuna watu wako Maneromango huko unakuta wanapotosha kwamba bandari yetu imeuzwa wakati hawajawahi kufika hata bandarini, jamani bandari haiuzwi, inafanyiwa tu uwekezaji”