Mkoa wa Morogoro umeungana na Mikoa mingine katika kuadhimisha siku ya mashujaa ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe kama ya leo julai 25 ya kila mwaka.
Mkuu wa Mkoa Adam Malima ameongoza zoezi hilo la kumbukizi katika mnara wa mashujaa uliopo maeneo ya posta Mkoani humo ,ambapo amewaasa wakazi wa Morogoro kuendelea kulinda amani ya nchi.
Nae Chifu Kingalu kiongozi wa kimila kabila la Waluguru ameeleza mchango wa viongozi wa kimila kipindi vita inapiganwa hasa katika kuimarisha umoja na ushikamano .