Home KITAIFA MAPINDUZI YA MIUNDOMBINU YA UTALII KILWA KISIWANI YAWAACHA MIDOMO WAZI WATALII 120

MAPINDUZI YA MIUNDOMBINU YA UTALII KILWA KISIWANI YAWAACHA MIDOMO WAZI WATALII 120

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA imepokea jumla ya watalii 120 waliotembelea na kutalii katika hifadhi ya magofu ya kale Kilwa Kisiwani na kueleza kuridhishwa kwao na utalii wa kutumia boti la kisasa lenye kioo maalum kinachomwezesha mtalii kuona viumbe hai vilivyopo chini ya bahari iliyozinduliwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa

Watalii hao wamesema matarajio yao yamefikiwa kwa kiwango cha juu zaidi ya walivyofikiria awali kabla ya kufika katika hifadhi hiyo kutalii na kuliona boti hilo la Kisasa almaarufu TAWA Sea Cruiser .

TAWA inaendelea kuwahamasisha watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani kutembelea hifadhi hiyo kujionea mapinduzi ya utalii yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia wafurahie uzuri wa utalii wa baharini, kiutamaduni na kihistoria.

 

Previous articleMIRADI YA BILIONI 3.6 YAPITIWA NA MWENGE SAME
Next articleMADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA SHINYANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here