Home KITAIFA MAONESHO YA TEKNOLOJIA KUFUNGUA MILANGO YA KIUCHUMI MKOA WA GEITA

MAONESHO YA TEKNOLOJIA KUFUNGUA MILANGO YA KIUCHUMI MKOA WA GEITA

 

Na Joel Maduka Geita.

Maonesho ya Teknolojia ya Madini ya Kimataifa ambayo yanaendelea mjini Geita yanatarajia kuwakutanisha washiriki zaidi ya 400 yakiwemo makampuni ya ndani ya nchi na nje ya nchi lengo likiwa ni kuwezesha wachimbaji wadogo kutambua teknolojia ya kisasa ya uchimbaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, amesema kwa mwaka huu idadi ya washiriki imeongezeka kutoka 200 hadi kufikia 400 kutokana na wafanyabiashara ,makampuni mengi kuona umuhimu wa kushiriki maonesho ya madini.

Mkuu wa Mkoa Shigela pia ametaja mataifa ambayo yamethibitisha kushiriki kwenye maonesho hayo ni Kenya, Malawi, Burundi, China, India, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na wenyeji Tanzania.

“Tayari washiriki kutoka Burundi wameshawasili, wanaanza kutembelea maeneo ya wachimbaji wadogo, ni wachimbaji wadogo wameungana na serikali ya Burundi kuja kufanya matembezi hayo.Wanakuja kushiriki maonyesho haya ili wajifunze mambo mapya ya teknolojia, lakini na wenyewe wajifunze namna ya kuratibu maonyesho, na hivo kuwezesha nchi zao pia kuandaa maonyesho.” Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Shigela ameongeza , maonesho ya madini yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 23, na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.  Dotto Bitko na kufungwa na Rais Samia Suluhu Septemba 30, 2023.

Previous articleTANZANIA YAHIMIZA USAWA KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA
Next articleVIONGOZI TUJITAHIDI KUWA NA UBINADAMU NAKUFUATA MASHARTI YA KAZI ZETU- SIMBACHAWENE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here