Home KITAIFA MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO LA DHARURA AWASIHI WAUGUZI KUFANYA KAZI KWA...

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO LA DHARURA AWASIHI WAUGUZI KUFANYA KAZI KWA WELEDI

 

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa madaktari na watoa huduma wote kuendelea kufanya kazi kwa kujituma, upendo, kujitoa na kuzingatia weledi na maadili ya tasnia ya utabibu ili kuokoa maisha ya Watanzania.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Jengo la Huduma za Dharura (EMD) katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha.

Dkt Mpango Amesema viongozi wa hospitali hiyo wanapaswa kutoa umuhimu mkubwa katika kutunza vifaa tiba kwa kuhakikisha vinafanyiwa ukarabati kwa wakati ili vidumu kwa muda mrefu.

Amesema serikali inatarajia kukabidhi magari mawili ya wagonjwa katika hospitali hiyo pamoja na madaktari zaidi ya 25 kwa Wilaya ya Arumeru ikiwa ni njia ya kukabiliana na changamoto za upungufu wa rasilimali watu katika sekta ya afya wilayani humo.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali za mara kwa mara zinazogharimu maisha ya wananchi.

Dkt Mpango Amesema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofikishwa katika huduma za dharura wanatokana na ajali hivyo amelisihi jeshi la polisi kusimamia sheria zilizowekwa kikamilifu ili kuendelea kupunguza adha ya ajali nchini.

Previous articleWIZARA YA MADINI YASISITIZA KUENDELEA KUWALEA WACHIMBAJI WADOGO
Next articleRAIS SAMIA AIPONGEZA YANGA KWA KUWAJAZA MANOTI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here