Home KITAIFA MAKAMBA: MWENGE WA UHURU NI TUNU YA TAIFA

MAKAMBA: MWENGE WA UHURU NI TUNU YA TAIFA

Waziri wa Nishati January Makamba amesema kuwa,  kumekuwa na hoja na mjadala kwabaadhi ya wanasiasa hasa wa upande wapili wakidai mwenge wa uhuru umepitwa na wakati.

Makamba amesema kuwa Mwenge ni Tunu ni nembo ya Taifa hivyo na kwa kusema mwenge unasumbua watu ni sawa na kuitusi nchi ya Tanzania.

Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ameyasema hayo mara baada ya mwenge kufika katika Jimbo hilo, ambapo mwenge huo umezindua na kukagua miradi 9 yenye thamani ya sh.779.1 milioni

“Tukiwa na mawazo na mtazamo huo tunaitusi historia ya nchi yetu kwani nchi yetu ilipopata uhuru, hotuba ya kwanza ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere amesema sasa tunawasha mwenge iliuangaze nchi nzima,” amesema January Makamba

Alisisitiza kuwa mwenge wa uhuru ni kielelezo cha uhuru, utaifa wetu, ni ndoto zetu, na ni kiunganishi cha watanzania pamoja na kuwa utamaduni na kielelezo cha utaifa wa Tanzania.

Alifafanua kuwa kila nchi ina urithi wake na utamaduni zake na kila ukoo una tamaduni zake na kwamba kwa Tanzania moja ya urithi wake ni Mwenge na ndiyo maana upo kwenye nembo ya taifa na hata kwenye sarafu.

Previous articleUVCCM YASHTUKIA JANJA YA UPINZANI, YAWAJIA JUU WANAOTOA KAULI ZA UBAGUZI
Next articleNEC YATAKANGAZA UCHAGUZI MDOGO KATIKA KATA 14

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here