Home KITAIFA MAJALIWA AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

MAJALIWA AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka madereva wote wa Serikali na Taasisi zake kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani na sheria za nchi katika uendeshaji wa gari huku akidai kuendesha gari la serikali haimaanishi wamepewa rungu la kuvunja sheria huku akiwataka kuwa mfano wa kuzingatia sheria za nchi kuhusu usalama barabarani.

Pia amewataka Maafisa masuhuli na Vyombo vya usalama kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji na kuchukua hatua kuhusu taarifa za baadhi ya madereva kujihusisha na wizi wa mafuta kwa kudanganya taarifa za umbali au kuuza mafuta kupitia vituo vya mafuta au kutoka katika magari yao na kuongeza kuwa Vitendo hivi ni ukiukwaji wa masharti ya ajira na uhujumu kwa Serikali.

Waziri Majaliwa ametoa maagizo hayo Agosti 7, 2023 jijini Dodoma wakati wa hafla Kukabidhi magari na vifaa vya kazi vya ofisi za Mikoa za idara ya kazi na wakala wa usalama na afya mahali pa kazi Vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 4.3.

Majaliwa amesema amesema Magari ya Serikali yatumike kwa shughuli za umma tu badala ya shughuli binafsi.

‘’Maafisa Usafiri katika Idara zote za Serikali wazingatie mpango maalum wa matengenezo ya magari kufanyika kwa wakati, kutumia vifaa vyenye ubora na kutunza taarifa za kila chombo. Hii itapunguza idadi ya magari yanayowekwa kwenye maegesho kwa muda mrefu ikiwemo katika karakana za Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),Aidha, ifikapo tarehe 30 Oktoba, 2023 Taasisi zote zenye magari yaliyoogeshwa kwa muda mrefu TEMESA yawe yametengenezwa na kuondolewa na nipate taarifa,’’

Pamoja na hayo amewataka Watumishi wa umma katika ngazi mbalimbali kuhakikisha kero za wananchi zilizopo katika maeneo yao zinatatuliwa ili wananchi kutolazimika kwenda ngazi za juu au kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa kwa masuala ambayo yangeweza kufanyiwa kazi kwa nafasi zao.

‘’Watumishi wa umma tengeni muda wa kwenda kusikiliza kero za wananchi katika maeneo yao badala ya kukaa ofisini muda wote. Aidha, wananchi wanaofika ofisini wasikilizwe na kuhudumiwa kwa wakati na kuwapa majibu ili wasipoteze muda mwingi kufuatilia majibu ya hoja zao,’’.

Previous articleHUKUMU KESI YA BANDARI YAPIGWA KALENDA
Next articleDC JOKATE AWAPONGEZA AKINA MAMA WANAOZALISHA MAZAO YA ASILI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here