Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Kinondoni imeiamrisha hospitali ya Muhimbili kuwapima watuhumiwa watatu kama wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Amri hiyo imetolewa jana Aprili 20,2023 na kusainiwa na Hakimu Mkazi J. J Rugemalila ikiwataja watuhumiwa wanaotakiwa kupimwa kuwa ni Noel Ndale Mushi, Kelvin Maliki Ngao na David Brayan Johnson anayedaiwa kuwa ni raia wa kigeni.
Hali hiyo ni katika moja ya kukusanya ushahidi (exhibit) wa shauri Na. 4/2023, Jamhuri dhidi ya watuhumiwa wote watatu.
Hatua hii inakuja ikiwa ni wiki chache tangu kuibuka kwa madai ya kushamiri kwa vitendo vya ushoga na usagaji nchini ambapo hivi karibuni serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, ilisema itapambana vikali dhidi ya vitendo hivyo.