Home KITAIFA MAGARI YA KENYA YAKIMBILIA TANZANIA KUFUATA BEI NAFUU YA MAFUTA

MAGARI YA KENYA YAKIMBILIA TANZANIA KUFUATA BEI NAFUU YA MAFUTA

Gharama kubwa ya mafuta nchini Kenya ambayo inawafanya madereva kwenda Tanzania kutafuta bidhaa hiyo muhimu inapelekea vituo vya mafuta katika nchi ya Tanzania karibu na mpaka wa Tanzania na Kenya kaunti za Isbania na Migori kupokea wateja wengi zaidi kutoka nchi jirani ya Kenya kutokana na mahitaji makubwa kutoka kwa wateja wa Kenya.

Kituo cha televisheni cha Citizen kutoka nchini Kenya, kimeeleza kuwa, hivi karibuni kumeshuhudiwa msongamano mkubwa wa magari na bodaboda katika barabara kuu ya Isbania na Migori inayoelekea mpaka wa Kenya na Tanzania unaopatikana katika mji wa Isbania kununua mafuta huku watumiaji wa vyombo hivyo vya moto wakieleza kuwa huko waendako (Tanzania) kuna mafuta ya kutosha lakini pia bei yake ni nafuu ikilinganishwa na watokako.

Katika mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo Isbania, kumeshuhudiwa madereva wa Kenya na waendesha bodaboda wakihangaika kuvuka kila mara katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) kwenda kununua mafuta ya bei nafuu upande wa Tanzania.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, wahudumu katika vituo vya kujazia mafuta upande wa Tanzania wameeleza kuwa, wamekuwa wakipokea wateja wengi kutoka nchi jirani ya Kenya na kueleza kuwa sababu kubwa ni unafuu wa bei lakini uwepo wa mafuta ya kutosha.

Aidha, wamesema mzunguko wa uuzaji wa mafuta kwa sasa umekuwa mkubwa kwani kila baada ya siku mbili gari ya mafuta inaleta mafuta kutokana na mahitaji kuwa makubwa

“Watu wengi sana wanapenda kuja kujaza mafuta hapa Isbania (upande wa Tanzania) na wengi wao ni kutoka Kenya” alisema muhudumu Carol Joseph

Kwa upande wake muhudumu Esther Emannuel amesema

“Tukileta mafuta inachukua muda mfupi kuisha, hii inatokana na bei nzuri na wateja wengi, jana yameisha na leo gari iko njiani kuleta mafuta”

Kwa upande wake Carol Joseph amesema,

“Watu wengi sana wanapenda kuja kujaza mafuta hapa Isbania (Upande wa Tanzania), na wengi wao ni kutoka Kenya”

Kwa upande wao, madereva bodaboda eneo la mpakani upande wa Kenya wameeleza sababu ya wao kukimbilia upande wa Tanzania huku sababu kuu ikiwa ni unafuu wa bei

“Tunakimbilia Tanzania kununua mafuta kwa kuwa Kenya kuna uhaba wa mafuta na pia bei iko juu” Mwita Maswi, bodaboda Isbania

“Bei ya mafuta imekuwa ni pigo hususan kwa vijana ambao wanajishughulisha na bodaboda” Bahati Joseph, bodaboda Isbania

Katika hali ya kushangaza, uchunguzi mdogo uliofanywa na mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni ya Citizen ya nchini Kenya, Seth Olale umeeleza kuwa vituo vya kujazia mafuta vya upande wa Kenya ambavyo vipo karibu na mpakani mwa Tanzania na Kenya upande wa Kenya vilivyopo kilometa chache toka mpakani havina wateja huku wateja wengi ambao ni bodaboda na watumiaji wa vyombo vya moto wakisafiri hadi upande wa Tanzania kufuata bidhaa hiyo muhimu.

Watumiaji wa vyombo vya moto nchini Kenya wameiomba wameiomba serikali yao kushughulikia sakata la kupanda kwa bei ya mafuta ili kupunguza makali ya maisha na kufanya wananchi wawe na maisha bora.

Lita moja ya mafuta upande wa Tanzania (mpakani mwa Kenya na Tanzania-Isbania) ni shilingi 3500 sawa na shilingi za Kenya 170 huku nchini Kenya yakiuzwa kuanzia shilingi 213.50 kwa lita

Previous articleMABILIONI YA MIRADI YAWAPONZA VIGOGO UVINZA, MAJALIWA AAGIZA TAKUKURU ‘WALE NAO SAHANI MOJA’_ MAGAZETINI LEO IJUMAA SEPTEMBA 22/2023
Next articleWACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UTAFITI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here