Home KITAIFA MABALOZI WA TANZANIA NJE YA NCHI KUIBEBA SEKTA YA MADINI

MABALOZI WA TANZANIA NJE YA NCHI KUIBEBA SEKTA YA MADINI

Leo Agosti 30, 2023 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewapokea Waheshimiwa Mabalozi Wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania nchini Canada, Namibia, Austria, Oman na Ufaransa jijini Dodoma.

Ziara hiyo ya Mabalozi imelenga kufahamishwa kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini nchini.

Katika kikao hicho Mabalozi watapata taarifa kutoka katika taasisi za Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Taasisi za Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), STAMICO, TEITI na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Mabalozi hao waliotembelea Wizara ya Madini ni Balozi Joseph Sokoine anayekwenda Canada, Balozi Fatma Rajab- anayekwenda Oman, Balozi Naimi Azizi- anayekwenda Austria, Balozi Ali Jabir Mwadini – anayekwenda Ufaransa na Balozi Ceaser Waitara -anayekwenda Namibia

Previous articleZAHANATI ZA KATA YA MKANGE HAZINA MANESI
Next articleMBUNGE MCHUNGAHELA AWAKINGIA KIFUA WANAWAKE NA VIJANA WACHIMBAJI MADINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here