Home KITAIFA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMONDO KUFANYIKA MBOZI MKOANI SONGWE

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMONDO KUFANYIKA MBOZI MKOANI SONGWE

 

Kassim Nyaki na John Mapepele, Arusha.

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatarajia kufanya maadhimisho ya siku ya Kimondo duniani ambayo itafanyika eneo la Kimondo cha Mbozi, Mkoani Songwe kuanzia Juni 26 – 30, 2023.

Kwa mujibu wa wataalam wa anga, Kimondo cha Mbozi chenye uzito wa tani 16, urefu wa futi 9.80, kimo cha futi 3.30 na upana wa futi 3.30 kwa mara ya kwanza kiligunduliwa na Mzee Halele mkazi wa Kijiji cha Ndolezi kutoka kabila za Wanyiha na baadaye Kimondo hicho kuwekwa katika maandishi na mpelelezi William Nott mwaka 1930.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohammed Mchengerwa amesema
Iengo la maadhimisho ya siku ya Kimondo ni kuendeleza uhifadhi wa urithi wa anga, kuendeleza sayansi na elimu ya anga kwa jamii pamoja na kutangaza zao jipya la utalii wa Anga ( *Astro tourism).*

“Maadhimisho haya yanaenda sambamba na kutambulisha zao jipya la utalii wa anga (astro tourism). Hii ni sehemu ya mkakati wa Wizara kendelea kubuni mazao mapya utalii na kutangaza vivutio vilivyoko mikoa ya kusini, natoa rai kwa wakuu wa Mikoa hiyo na wakuu wa Wilaya kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko mikoa hiyo ili wananchi waijue na kuwa mabalozi kwa wageni wengine wa kimataifa” amefafanua Mhe. Mchengerwa.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa maadhimisho ya siku kimondo yataambatana na programu mbalimbali ikiwemo kongamano la kimataifa la wanasayansi na wabobezi kuhusiana na elimu na utalii wa anga, utoaji wa elimu kwa jamii pamoja na shule za msingi na Sekondari Wilayani Mbozi.

Programu nyingine ni pamoja na kufanya shughuli za utamaduni, michezo na mbio za Kimondo ( _Kimondo marathon_ ), kupata simulizi kutoka kwa wenyeji kuhusiana na matumizi ya kimondo katika maisha na tamaduni zao pamoja kushindanisha wanafunzi katika ubunifu wa kutengeneza maumbile ya urithi na utalii wa anga.

Previous articleTANZANIA, UINGEREZA KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA
Next articleKITUO CHA UTALII KUJENGWA KIHESA – KILOLO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here