Home KITAIFA KUNA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE KINACHOCHEA MGOMO WA WAFANYABIASHARA KARIAKOO-MWENYEKITI WA WAFANYABIASHA...

KUNA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE KINACHOCHEA MGOMO WA WAFANYABIASHARA KARIAKOO-MWENYEKITI WA WAFANYABIASHA KARIAKOO

Imebainika kuwa kuna kikundi cha watu wachache Wahuni wanaoendesha mgomo wa wafanyabishara wa Kariakoo Jijinj Dar-esSalaam, hasa wale ambao wameendelea na Mgomo leo kwa lengo kuonesha Serikali haiwasikilizi Wananchi na kumchafua Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa Kariakoo Martin Mbwana wakati akizungumza na waandishi wa habari wa habari mapema leo Mei 16- 2023 waliomuhoji kwa nini baadhi ya wafanyabiashara wameendelea na mgomo leo wakati jana baada ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa kufika Kariakoo na kuzungumza nao walikubali kufungua maduka yao.

“Kariakoo mpaka leo asubuhi hali ilikuwa shwari, hali ilibadilika baada ya kutokea kikundi cha watu wachache wenye Maslahi yao binafsi, kupita chini chini na kuhamasisha mgomo, mimi jana nilizungumza nao na wakakubali kufungua Maduka yao” Amesema mwenyekiti huyo.

Amesema “mgomo ulianza jana, Bahati Nzuri Mama, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni Msikivu, alimuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akaja Kariakoo tunazungumza naye sisi Viongozi, tukakubaliana akaongee na Wafanyabiasha, akakubali akaongea nao akaomba akitoka kwenye Msiba [Wa Benard Membe] atarudi kutatua kero za Wafanyabiasha kesho Jumatano pale anatoglo tuyazungumza sasa Nashangaa Wafanyabiasha hao wamegoma leo”

Ameeleza kuwa “Tumepaza sauti Mhe. Rais amesikia amemtuma mtendaji wake Mkuu [ Waziri Mkuu] naye amefika, akatuomba fungueni Maduka Jumatano anakuja tuyazungumza, sasa mnataka nani mwingine aje ndiyo mmsikie? Amehoji Mwenyekiti huyo.

Ameongeza kuwa shida sio Viongozi au Wafanyabiasha, bali ni kikundi cha watu wajanja wanaoendesha Jumuiya zao kwa kutaka kujinufaisha na huo mgomo au wanataka kuonesha kwamba Serikali ya Rais Samia haisikilizi watu, hivyo ameomba vyombo vya dola vifanye kazi yake katika kwa wale ambao wanakaidi makubaliano waliyoingia jana na kutaka kuendelea na mgomo.

Aidha licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwatangazia Wafanyabiasha hao atakutana nao kesho Jumatano kushughulikia kero zao, tayari alishaanza kuchukua hatua za awali ikiwemo kuiagiza Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kusitisha matumizi ya kikosi maalum “Task Force” ambacho kilikuwa kinaendesha zoezi la ukamataji wa wafanyabiashara katika soko la kimataifa la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Previous articleSERIKALI KUSHIRIKISHA WANANCHI KUHUSU KUONDOLEWA KWA KIJIJI CHA NGARESERO KWENYE PORI TENGEFU LA POLOLET, NGORONGORO
Next articleMDEE AJIBU MAPIGO YA MAANDAMANO BAWACHA _MAGAZETINI LEO JUMATANO MEI 17/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here