Na _Dishon Linus_
Onana alikamilisha uhamisho wake wa awali wa £44m kwenda Old Trafford siku ya alhamisi, mara moja akasafiri kwa ndege kwenda New York kuungana na kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu kwa ziara yao ya Marekani.
Hapo awali United hawakuwa wamepanga kumnunua golikipa mpya msimu huu wa joto, lakini baada ya mazungumzo ya mkataba na David de Gea kushindikana na kuondoka klabuni hapo kwa uhamisho wa bure mwanzoni mwa Julai, walilazimika kurejea sokoni.
Onana aliibuka kama gorikipa wao mkuu na ataungana tena na Ten Hag waliowahi kufanya kazi pamoja Ajax. Akizungumza na wandishi wa habari wa klabu ya United, Ten Hag alizungumzia sifa za Onana na kwa nini alitaka kumsajili tena.
“Kwangu mimi Onana ni moja ya magorikipa ninao wahusudu sana barani ulaya na nimefanya nae kazi nikiwa Ajax hivyo namfahamu vizuri,naamini ataweza mfumo wangu msimu ujao”