Home KITAIFA KINANA: CHAMA KITAISHAURI SERIKALI KUANGALIA UPYA SHERIA YA BODABODA

KINANA: CHAMA KITAISHAURI SERIKALI KUANGALIA UPYA SHERIA YA BODABODA

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaishauri serikali iwasikilize wananchi inapotaka kutengeneza sheria mbalimbali zinazogusa maisha yao ili kupunguza migogoro na kero mbalimbali katika jamii.

Akizungumza leo Julai 27, 2023 baada ya kupokelewa wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amesema upo umuhimu wa kuangaliwa upya kwa sheria zinazowaumiza wananchi kama Ile ya usafiri wa bodaboda ambayo kwa sasa inakataza kubeba abiria zaidi ya mmoja.

“CCM inakwenda kuzungumza na serikali kuiangalia sheria ya usafiri wa pikipiki (bodaboda) ili iruhusu kubeba abiria zaidi ya mmoja,” amesema.

Awali jana akiwa Musoma mkoani Mara, Kinana ameeleza kwa kina kuhusu suala la bodaboda kubeba abiria zaidi ya mmoja na wajasiliamali wadogo kunyanyaswa na Mamlaka mbalimbali kutokana na Sheria zilizopo.

Akifafanua kuhusu usafiri wa bodaboda, Kinana amesema nchi nyingi duniani wananchi wake wanaotumia usafiri huo na kuruhusu kubeba abiria zaidi ya mmoja.

Previous articleDAWA ITAKAYOKUSAIDIA KUWA KIONGOZI AU MWANASIASA MZURI
Next articleMAMIA YA WAKAZI WA KIJIJI CHA REMG’ORORI SERENGETI WAANDAMANA KUSHINIKIZA SERIKALI IMALIZE MGOGORO WA MIPAKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here