



Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (kushoto) akimkabidhi zawadi Rais mstaafu Jakaya Kikwete kutokana na mchango wake kwenye Kampeni ya GGML Kili Challenge iliyoanzishwa na kampuni hiyo mwaka 2002 kwa kushirikiana na TACAIDS. Jana Alhamisi Kikwete ameshiriki katika uzinduzi wa harambee ya kampeni hiyo kwa mwala huu jijini Dar es salaam
JUMLA ya Dola za Marekani 700,000 (sawa na Sh bilioni 1.6) zimepatikana katika uzinduzi wa harambee Ya kampeni ya GGML Kili Challenge iliyoongozwa na Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kwa lengo la kukusanya Sh bilioni 2.3 fedha zitakazotumika kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Kampeni hiyo iliyoasisiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ilianzishwa mwaka 2002 na kufikia makundi mbalimbali yaliyo katika maeneo hatarishi kwenye janga hilo.
Akizunguma katika harambee hiyo iliyofanyika jana tarehe 18 Mei 2023 jijini Dar es Salaam, Dk. Kikwete aliipongeza GGML na TACAIDS kwa ushirikiano walioufanya na kuanzisha kampeni hiyo inayounga mkono jitihada za Serikali kudhibiti maambukizi ya VVU/ UKIMWI.
“Endeleeni kuitangaza GGM Kili Challenge kwa kupitia mabalozi mbalimbali na celebrity (watu maarufu) ili kampeni hii iwe jambo linalozungumzwa duniani,” alisema.
Tanzania bila UKIMWI, inawezekana! Msemo huo ulikuwa wa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong mbali na kuishukuru Serikali kwa kuunga mkono kampeni ya GGML Kili Challenge alisema wakiwa wadau wa mapambano hayo ya UKIMWI na VVU, GGML imepokea msaada ambao uliiwezesha Kili Challenge kupiga hatua kubwa hadi kufikia kuwa mfuko wa kimataifa, wenye kushirikisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.
Kwa upande wake Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo amesema tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo makundi mbalimbali yamefaidika ikiwa kuazishwa kwa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu – Moyo wa Huruma kilichopo Geita.