Home KITAIFA KIKONGWE AUAWA KWA KUKATWAKATWA MAPANGA DODOMA

KIKONGWE AUAWA KWA KUKATWAKATWA MAPANGA DODOMA

 

MWANAMKE mmoja anayefahamika kwa jina Mariam Mdachi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 95 hadi 100 julai mosi mwaka 2023 ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kijana aliyefahamika kwa jina la Yohana Luhanga miaka 30 akidaiwa kukataza kukatwa kwa Makuti.

Tukio hilo limetokea katika Kata ya Kikuyu mtaa wa Mrasa ambapo chanzo cha mauaji kikidaiwa kukataza kukatwa kwa Mkuti na mtuhumiwa Yohana naye akijeruhiwa na watu wenye hasira kali.

Akizungumza Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dokta Samweli Magesa amesema kuwa mnamo Julai 1 ,mwaka 2023 majira ya saa 6 za mchana walipokea maiti moja na majeruhi mmoja aliyekuwa na umri wa zaidi ya miaka 30.

“Katika uchunguzi wetu tuliofanya mwili huo ulikuwa na majeraha katika mwili wake ambapo ulisababisha na kukatwa na kitu chenye ncha kali katika maeneo mbalimbali”alisema.

Akitaja sababu iliyopelekea kifo cha mama huyo Dk.Magesa amesema ni kuvuja kwa damu nyingi kutokana na majeraha makubwa ambayo aliyapata lakini pia kijana huyo ambaye alifanya mauaji hayo naye alipata majeraha katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ,kama kwenye kichwa na baadhi ya sehemu mbazo zilikuwa zinavuja damu.

“Tulifanikiwa kumpa huduma ambazo zilitakiwa na tumemlaza wodini na kwataarifa nilizonazo ni kwamba anaendelea vizuri lakini uchunguzi bado utaendelea kwajinsi tutakavyokuwa tunaendelea kumuhudumia”alisema Dk.Magesa.

Pamoja na hayo amesema kuwa kwa taarifa walizonazo kijana huyo ambaye yupo chini ya uangalizi alijeruhiwa na wananchi wenye hasira kali.

Naye mmoja wa mashahidi aliyekuwa katika eneo la tukio Neema Swai amesema kuwa tukio hilo limemgusa sana kwani huwa anapita karibu na anapokaa bibi huyo wakati akienda mjini ambapo mara nyingi alikuwa akimkuta akiwa na jembe lake analima.

Tunaomba serikali ilete ulinzi shirikishi kwani kungekuwepo na kituo cha polisi basi bibi wa watu asingeweza kuuliwa.

Petro Chibago ambaye ni mkazi wa eneo hilo amesema kuwa kijana huyo aliyefanya mauaji hayo huwa anatatizo la afya ya akiri ambapo huwa anaanguka kifafa na anafanya vitu vya kitofauti mtaani.

“Nilikuwa nimelala nikasikia makelele nilipotoka nje nikakutana na yohana nikaamua kukimbia kwani yohana anaogopeka”amesema

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Martin Otieno amekiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo limetokea katika mtaa wa mrasa kikuyu, ambapo mama mmoja mtu mzima anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 95 hadi 100 aliuawa kwa kupigwa na panga katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kichwani na kwenye mkono.

Amesema mtuhumiwa aliyefanya mauaji hayo aliyefahamika kwa jina la Yohana Luhanga ameshakamatwa lakini baada ya kufanya tukio hilo wananchi wenye hasira kali walijichukulia sheria mkononi na kumjeruhi vibaya kwenye mkono wake .

“Hivyo naye mtuhumiwa huyo alipelekwa hospitali kwaajili ya kufanyiwa matibabu na utaratibu unaendelea na ukishakamilika basi atafikishwa mahakamani”.

Akizungumzia chanzo cha tukio hilo Kamanda Otieno amesema mtuhumiwa Yohana alienda kwa mama huyo kuomba kukata kuti kwaajili ya kuchukua makuti,lakini mama huyo ambaye ni marehemu alimwambia hawezi kukata mwenyewe atafute na watu wengine ili waje wakate,baada ya kujibiwa hivyo mtuhumiwa huyo alipatwa na hasira na kuanza kumcharanga mama huyo kwenye mwili wake.

Previous articleTPSF ,UDSM YA SAINI MOU MWAROBAINI AJIRA ZA WAHITIMU WA VYUO
Next articleKESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI KUANZA KUUNGURUMA JULAI 20 MBEYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here