Home KITAIFA KIINI UKOSEFU WA HAKI KWA WALEMAVU CHATAJWA

KIINI UKOSEFU WA HAKI KWA WALEMAVU CHATAJWA

WADAU wa haki wamesema ukosefu wa miundombinu rafiki kwenye majengo ya vyombo vya utoaji haki pamoja wakalimani wa lugha ya alama kwa viziwi nchini ni moja ya vikwanzo vinavyopelekea walemavu kushindwa kupata haki zao.

Wadau hao wameyasema hayo Julai 19, 2023 Jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa wadau wa haki ulioandaliwa na Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwaajili ya kupitia taarifa juu ya kuimarisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Mkutano huo, Mdau wa masuala ya haki Enock Mbawa, amesema watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na kero mbalimbali katika vyombo vya utoaji haki nchini.

“Vyombo vya utoaji haki nchini kama Mahakama na Polisi bado kuna changamoto mbalimbali kwa watu wenye ulemavu, leo hii kama mlemavu anakesi lakini hana mkalimani wa kumsaidia kutafsili mambo mbalimbali ya kimahakama lazima ataachana na keshi hiyo hivyo kupoteza haki yake”alisema
Kutokana na hali hiyo aliiomba serikali kuwekeza nguvu kwenye miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu katika majengo yote yanayotumika kutoa haki.
“Lazima kuangalia kama katika vyombo vyetu vya utaoaji wa haki kama Mahakama na polisi kuwepo na uwezekano namna ya kumsaidia kisiwi kupata nyaraka za kesi ambazo anaweza kuzielewa ili kuweza kufuatilia haki yake vinginevyo akiona hana anacho kielewa lazima atakata tamaa na kuachana na kesi hiyo”amesema
Aidha, ameitaka serikali kutenga bajeti jumuishi ambayo itasaidia makundi ya watu wenye ulemabu nchini kupata haki sawa kama ilivyo kwa wananchi wengine.

Naye Mwenyekiti wa TLS, kanda ya kati Mary Munisi amesema lengo la kupitia ripoti hiyo ni kuisaidia serikali kufanya maboresho katika sheria pamoja na sera mbalimbali ili kuwezesha walemavu kufikiwa na huduma za vyombo vya utoaji haki nchini.
“Moja ya kazi ya TLS ni kuisaidia serikali kama kutahitajika kufanya maboresho kwenye sheria ya watu wenyeulemavu ya mwaka 2010 basi yafanyike ili kuboresha mambo ambayo yameonekana vikwazo kwa walemavu kupata haki nchini”alisema Munisi.

Kwa upande wake Ofisa ustawi wa jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha watu wenye ulemavu Bruno Mwakibibi, amesema lengo la kikao hicho ni kuangalia kero ambazo wanakumbana nazo walemavu kupata haki kwenye vyombo hivyo.

Amesema bado zipo kero mbalimbali ambazo zinawanyima watu wenye ulemavu kupata haki zao katika vyombo vya utoaji haki ikiwemo miundombinu isiyo rafiki kwao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawakili na Wanasheria wenye ulemavu wa TLS, Gidion Mendes, alisema kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, asilimia kumi ya watu kati ya watanzania zaidi ya milioni 61 ni walemavu hivyo wanayo haki ya kupata huduma kama ilivyo kwa wengine.

Previous articleRC AWATAKA WADAU WA ELIMU KUUNGA MKONO UBORESHAJI WA ELIMU NCHINI
Next articleCANADA WATOA DOLA MILIONI 50 KWA AJILI YA MRADI WA KILA BINTI ASOME NA MPANGO WA AJIRA (UFUNDI STADI)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here