Home KITAIFA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI KUANZA KUUNGURUMA JULAI 20 MBEYA

KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI KUANZA KUUNGURUMA JULAI 20 MBEYA

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya inatarajia kuanza rasmi usikilizaji wa kesi ya kikatiba ya kupinga kusainiwa kwa mkataba wa Bandari iliyofunguliwa na wananchi wakiwakilishwa. A mawakili Boniface Mwabukusi, Livino Ngalimitumba na Philip Mwakilima wakisema mkataba huo hauna maslahi kwa Taifa.

Akizungumza mbele ya mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa, Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali Hangi Chang’a akisaidiana na mwenzake Ayubu Sanga ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasilisha majibu yao ya waleta maombi Boniface Mwabukusi na wenzake watatu.

Akijibu hilo Wakili wa wananchi Boniface Mwabukusi amesema shauri hilo limefunguliwa kwa hati ya dharura hivyo kuiomba mahakama kutoa tafsiri halisi ya maombi yao ambayo ni kupinga mkataba wa bandari ambayo Serikali inasema kilichopitishwa ni makubaliano na sio mkataba.

Mwabukusi anasema pia maombi yao ni kuona hakuna shughuli zinazoendelea ili kutoharibu kesi yao au msingi wa kesi yao kuharibika kusikoweza kutengenezeka.

“Hoja yetu (Kupinga kusainiwa kwa mkataba wa bandari) ni ya wananchi na Serikali ni Serikali kupoteza moja kwa moja rasilimali za umma”, Wakili Phillip Mwakilima mmoja wa mawakili wanaowawakikisha wananchi katika shauri hilo.

Walalamikaji ni pamoja na Wakili Emannuel Chengula, Alfonce Lusako, Raphael Ngonde na
Frank Nyalusi ambapo pia mwanaharakati Bob Chacha Wangwe amehudhuria mahakamani na kueleza kuwa hawatakaa wavumilie kuminywa haki na rasilimali za wananchi.

Mwabukusi amewaambia waandishi wa habari kuwa hawapingi uwekezaji bali wanapinga vifungu vilivyomo kwenye mkataba ambavyo wanadai si rafiki kwa wananchi huku akisema spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Wizara ya Ujenzi na uchukuzi wanatakiwa kujitafakari na kushinikizwa kuachia nafasi zao.

Jaji Dastan B. Ndunguru ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 14 kwa ajili ya jamhuri kutoa majibu ya waleta maombi na baadaye waleta maombi kujibu ikiwa watakuwa na hoja kisha shauri hilo kuanza kusikilizwa Julai 20, 2023 na linatarajiwa kusikilizwa na majaji watatu.

 

Previous articleKIKONGWE AUAWA KWA KUKATWAKATWA MAPANGA DODOMA
Next articleTUTOKOMEZE NDOA ZA UTOTO KWA UMOJA WETU- SERIKALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here