Home KITAIFA KESI YA BABA KUTUHUMIWA KUMBAKA, KUMLAWITI MWANAYE YAENDELEA

KESI YA BABA KUTUHUMIWA KUMBAKA, KUMLAWITI MWANAYE YAENDELEA

 

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mahakama ya Hakimu Mfawidhi mkoani Mbeya imeendelea kusikiliza kesi ya unajisi inayomkabili Mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Lyoto Kata ya Ilemi Jijini Mbeya akituhumiwa kumbaka na kumwingilia kinyume cha maumbile mtoto wake (09).

Akitoa ushahidi wake mbele ya mahakama kwa kuongozwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Emelda Aluko Shahidi wa Jamuhuri Erica Petro (25) mfanyabiashara mdogo wa Lyoto Ilemi ameiambia mahakama kuwa akiwa katika eneo lake la biashara huko Lyoto alifikiwa na dereva bodaboda asiyemfahamu akiwa amembeba mtoto aliyebakwa akiuliza ikiwa anamfahamu.

Shahidi Erica amesema kwakuwa alikuwa anamfahamu mtoto huyo aliongozana na dereva huyo hadi nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo ambaye baada ya kuhojiwa alidai amekutwa Iwambi na bodaboda huyo akitembea kuelekea kwa bibi yake Mbozi mkoani Songwe kwa maelezo kuwa amekuwa akibakwa na baba yake na kutishiwa kupigwa na kuuawa ikiwa atasema kwa mtu yeyote kitendo ambacho baba yake alikanusha vikali.

Hata hivyo shahidi huyo amesema baadaye mama mzazi wa mtoto huyo alienda kituo cha kutolea huduma ili kumfanyia vipimo mwanaye huyo mdogo na kubainika kubakwa na kuingiliwa kinyume cha kimaumbile ya asili ya mwanadamu.

Alipopewa nafasi ya kuhoji maswali kwa shahidi huyo mshtakiwa James Jonas ambalo si jina lake halisi (45) amehoji kwanini mtoto huyo akutwe Iwambi ikiwa kweli alibakwa lakini jamuhuri kupitia shahidi Erica Petro imesema alikutwa akitembea kwenda Mbozi ili kuepuka kadhia ya kunajisiwa na babaye mzazi.

Hata hivyo Mwendesha mashtaka wa Serikali Emelda Aluko na mwenzake George Ngwembe wameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine kwa ajili ya kuhitimisha ushahidi wao kisha kufunga shauri lao.

Hakimu Mfawidhi mkoa wa Mbeya katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Zawadi Laizer anayesikiliza kesi hiyo ameahirisha shauri hilo namba 6/2023 hadi Juni 13, 2023 na mshtakiwa amerudishwa mahabusu hadi tarehe tajwa.

Mshtakiwa huyo ambaye ni Mfanyabiashara anashtakiwa na jamhuri kwa tuhuma ya makosa mawili ya ubakaji wa mtoto huyo kosa ambalo ni kinyume na kifungu namba 130 (1), (2) (e) na 131 (1), (3) sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 na pili anadaiwa kumlawiti binti huyo kitendo kinachoelezwa kuwa kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) na (2) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

 

Previous article“NHIF YAELEKEZWA KUTOA HUDUMA MPAKA NGAZI YA ZAHANATI NA WAF- MHE GODWIN MOLLEL
Next articleWAKAZI WA IGANJO WALIA NA SERIKALI KERO YA BARABARA, MAJI, UMEME NA HUDUMA ZA AFYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here