Home KITAIFA KERO ZA RUSHWA KWA WANANCHI ZAMUIBUA SIMBACHAWENE KWA TAKUKURU

KERO ZA RUSHWA KWA WANANCHI ZAMUIBUA SIMBACHAWENE KWA TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeagizwa kuhakikisha inakuwa na mfumo wa kisheria na kiutendaji wa kudhibiti rushwa hasa rushwa ndogo ndogo ambazo zimekuwa kero kwa wananchi.

Agizo hilo limetolewa Novemba 20 , 2023 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Taasisi hiyo.

Simbachawene amesema rushwa hiyo imekuwa kero kwa wananchi hasa wanapohitaji kupata huduma katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za elimu,afya ,ofisi za kodi na kwenye utoaji wa leseni.

Aidha Simbachawene amewataka pia kutumia mkutano huo kujadili changamoto zinazowakabili ndani na nje ya taasisi kwa uwazi ili kuweza kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Salum Rashid Hamduni ameeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka mmoja ikiwemo kuokoa zaidi ya Shilingi Bilioni 171,kupitia operesheni mbalimbali walizozifanya.

Mkutano huo wa siku 3 umebeba kauli mbiu isemayo kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu ukiwa na lengo la kujadili utendaji kazi wao kwa kuangalia mafanikio,changamoto walizopata na kuweka mikakati ili kuboresha utendaji wao wa kazi kwa miaka ijayo.

Previous articleDC SHEKIMWERI AZITAKA OFISI ZA TAIFA ZA TAKWIMU AFRIKA ZIZALISHE TAKWIMU ZENYE UBORA
Next articleDC KATWALE AFUNGUKA JUU YA TETESI ZA WANYAMA KUTOWEKA HIFADHI YA BURIGI CHATO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here