Leo tarehe 15 Mei, 2023 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amefungua Ukumbi wa Mikutano wa CCM na Kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Nyumba ya Kupumzikia Viongozi (Rest House) wilayani Bukombe Mkoani Geita.
Miongoni mwa Viongozi walioshiriki katika zoezi hilo ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt Dotto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela, Mkuu wakuu wa wilaya, wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chama na serikali.
Miradi hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 200, fedha kutoka katika Michango ya wanachama wa chama hicho katika wilaya hiyo.