Home KITAIFA KATIBU MKUU NISHATI ASISITIZA GST KUFANYA UTAFITI ZAIDI

KATIBU MKUU NISHATI ASISITIZA GST KUFANYA UTAFITI ZAIDI

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesisitiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuendelea kufanya tafiti zaidi ikiwemo kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu uwepo wa madini mbalimbali nchini

Mhandisi Mramba amebainisha hayo leo Julai 3, 2023 alipotembea banda la Wizara ya Madini, Taasisi za Wizara na Wadau wa Sekta ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Aidha, ameishauri GST kusambaza vitabu vya Madini yapatikanayo Tanzania toleo Jipya 2023 kwa wananchi ili waweze kutumia taarifa hizo ambazo ni muhimu.

Mbali na GST ametembelea washiriki mbalimbali katika Banda la Wizara.

Previous articleWAKULIMA WATAKIWA KUTUNZA CHAKULA MARA BAADA YA MAVUNO
Next articleCHADEMA YATAKA RASILIMALI ZA NCHI ZIWANUFAISHE WANANCHI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here