Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana ,ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi ametoa maagizo kwa wakurugenzi wakuu wa mifuko miwili ya hifadhi ya jamii Tanzania PSSSF na NSSF Kuhakikisha wanashughulikia changamoto kwa baadhi ya waajiri ambao hawawasilishi michango ya watumishi wao.
Akizungumza na waandishi wa habari juni 20,2023 Dodoma Katambi amesema pamoja na kuvunja sheria ya kutowasilisha michango na wengine kuwasilisha michango pungufu hali hiyo inaleta usumbufu kwa wastaafu nanikinyume na sheria ya ajira na mahusiano kazini no 6 ya mwaka 2004
Aidha Katambi amewataka mameneja wote wa mikoa kuhakikisha wanasikiliza na kutoa elimu kuhusu taarifa za wanachama.
Aidha katambi amewataka waajiri wote kuhakikisha wanawasilisha taarifa za kustaafu mtumishi wake miezi sita kabla ya tarehe ya kustaafu ili kupunguza ucheleweshaji.