11 OCTOBER 2023
Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Njelu Kasaka* amemalizia ziara yake ya kata kwa kata na leo amewafikia wana Ifumbo na kutembelea vijiji viwili vya Lupa Market pamoja na Ifumbo.
Katika ziara yake Mhe.Mbunge ameweza kuongea na wananchi na kuwapa mrejesho wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo Kata ya Ifumbo imeweza kufaidika katika sekta ya miundombinu ya Barabara, Upatikanaji wa maji, pamoja na ujenzi wa zahanati na uboreshwaji wa zahanati ya Ifumbo.
Mhe.Kasaka pia amesikia changamoto za wana Ifumbo ambapo kilio chao kikubwa ni kusimamishwa kwa mwekezaji raia wa China, kuacha shughuli za uchimbaji pembezoni mwa mto Zilla.
Mhe. Kasaka amelipokea na ameahidi kulifikisha kwa mamlaka husika ili wana Ifumbo waweze pata suluhisho la kudumu kwa jambo hilo.