Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Mzee Ramadhan Nyamka Julai 5, 2023 amewasili Mkoani Ruvuma na kukagua miradi mbalimbalia ya Gereza Majimaji ikiwemo ujenzi wa nyumba za makazi ya maafisa na askari wa Gereza hilo.
Aidha CGP Nyamka amewapongeza maafisa na askari wa Gereza kwa kushirikiana na Mkuu wa Gereza katika kuendeleza na kubuni mradi huo.
Akitoa ripoti ya Gereza hilo mkuu wa Gereza Majimaji amemuomba Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza amtatulie changamoto ya maji kwa kuwachimbia kisima ili wapate uhakika wa maji safi na salama.