Home KITAIFA KAMERA KUFUNGWA KITONGA NA MAJINJA KUKABILIANA NA AJALI IRINGA

KAMERA KUFUNGWA KITONGA NA MAJINJA KUKABILIANA NA AJALI IRINGA

Ili kuepusha ajali za mara kwa mara katika Mkoa wa Iringa, uongozi wa mkoa Iringa kwa kushirikiana na jeshi la polisi umepanga mikakati maalumu ya kupunguza ajali za barabarani kwa kufunga kamera katika maeneo yote sumbufu,hasa eneo la Kitonga pamoja na eneo la Majinja.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas ametoa kauli hiyo Jumapili Agost 13, 2023 katika eneo la changarawe maarufu kama Majinja wilayani Mufindi wakati wa ziara ya kamati hiyo katika maeneo korofi.

Amesema kuwa tayari mchakato wa kutafuta wataalam kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu kwenye maeneo hayo umeanza na anaamini ikiwa kamera hizo zitawekwa kwenye maeneo hayo itakuwa mwanzo wa mageuzi ya barabra zingine nchi nzima kufanya jambo hilo.

Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Iringa Mosi Ndozero amepongeza juhudi hizo za kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa akisema kuwa pamoja na kuwekwa kwa kamera hizo jeshi la polisi linaendelea kuimarisha doria barabarani na kuwachukulia hatua madereva wanaovunja sheria.

Kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Imefanya ziara ya siku mbili katika maeneo korofi ya barabara za mkoa huo Ili kuangalia ufumbuzi wa kudumu katika maeneo korofi ya barabara ndani ya mkoa huo.

Previous articleWEZI WA MITIHANI WATANGAZIWA VITA, AWE MWANAFUNZI, MZAZI , MWENYE SHULE AU MWALIMU CHA MOTO ATAKIONA_ MAGAZETINI LEO JUMATATU AGOSTI 14/2023
Next articleVIJANA SIHA WASHAURIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here