Home KITAIFA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAFANYA ZIARA DUCE

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAFANYA ZIARA DUCE

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni,Sanaa na Michezo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Husna Sekiboko imefanya ziara katika Chuo kishiriki cha elimu DUCE ambapo pamoja na kazi zingine kamati imetembelea shule ya msingi Chang’ombe (Shule maalum ya serikali ya English Medium) iliyopo kwenye chuo hicho Jijini Dar Es Salaam.

Katika ziara hiyo walioifanya katika Shule ya Serikali ya mfumo wa Kiingereza (English medium) wameitaka serikali kutoa maelezo sahihi na elimu kwa umma juu ya uendeshwaji wa shule za aina hiyo zinazomilikiwa na Serikali.


Hii imetokana na hoja kwamba Serikali inatoa elimu bila malipo katika shule za msingi na sekondari nchini lakini shule za msingi za serikali za English Medium hutoza ada.

Aidha kamati imeitaka wizara ya elimu kukamilisha miradi ya vyumba vya madarasa na maabara kwenye shule hizo za DUCE ili majengo yaanze kutumika na kutoa tija inayokusudiwa.

Previous articleBODABODA AUAWA , ACHUNWA NGOZI _ MAGAZETINI LEO JUMATANO AGOSTI 09/2023
Next articleTSB KUZALISHA MKONGE TANI 60,000 MWAKA 2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here