Home KITAIFA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA TPA – MTWARA

Husna Hassan, Mtwara

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Moshi Selemani kwa niaba ya kamati hiyo amesema wameridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ya Mtwara.

Akizungumza Novemba 13, 2023 katika ziara yao ya kukagua miradi mbalimbali iliyopo mkoani Mtwara amesema kuwa wameshuhudia bandari mpya ambayo itahusika kubeba mizigo michafu kama makaa ya mawe na saruji ili kuepusha uharibifu wa mazingira ambao upo katika bandari inayotumika kwasasa pia kuepusha uharibifu unaoweza kuleta madhara kwa wananchi.

Pia Selemani amesema kwa sasa ongezeko la mapato kwenye bandari ya Mtwara ni makubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo kwasasa mapato yameongezeka kutoka bilioni 11 hadi bilioni 35 na kwa msimu huu upo uwezekano wa kufikia zaidi ya bilioni 40 kwasababu ya mzigo kuwa mkubwa.

Hata hivyo amewatoa hofu wananchi kwa kile kinachozungumzwa kuhusu uhaba wa makasha na kuwaambia kuwa wao kama kamati wamejiridhisha na jitihada za TPA i kwani makasha yapo mengi tofauti na malalamiko ya wananchi.

Ametoa wito kwa wananchi wa Kanda ya Kusini, Lindi,Ruvuma na Mtwara kutumia bandari ya hiyo kwani kadri inavyofanya kazi uchumi wa mkoa na taifa nao unaongezeka.

Previous articleMAAFISA TEHAMA WAPIGWA MSASA MFUMO WA GOTHoMIS
Next articleJUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA (JWT) YAHAMASISHA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI KWA HIYARI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here