Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Prof. Kitila Mkumbo leo Aprili 15, 2023 imetembelea Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa Tanzania (BMT) zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Baraza hilo katika uendelezaji wa Sekta ya Michezo hapa nchini.
Kamati hiyo pia imepokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidao ambapo imeoneshwa kuridhishwa na utendaji kazi wa BMT na TFF.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma, Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa, Wajumbe wa Kamati hiyo na baadhi ya Watendaji wa Wizara wamehudhuria.