Home KITAIFA KAMANDA MULIRO ATOA TAHADHARI KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA

KAMANDA MULIRO ATOA TAHADHARI KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limetahadharisha wale wanaofikiria kufanya uhalifu siku ya Sikukuu ya Pasaka waache mara Moja watashughulikiwa ipasavyo kwani Jeshi liko Imara kuhakikisha hali ya Usalama inakuwa shwari.

 

Kamanda wa Kanda Maalumu wa Dar es salaam SACP Jumanne Muliro amesema hayo akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaamo nakusema Polisi hawatasita Kufuatilia watu watakaotaka kupanga njama za kufanya uhalifu hawatalala kwani kila sikukuu kumekuwa na baadhi yao kutumia siku hivyo hivyo Jeshi litaendelea kufanya doria kila mahali.

Kamanda Muliro amesema hali ya Usalama katika Kanda ya Dar es salaam ni shwari ikilinganishwa na miaka ya nyuma kulikuwa na matukio mbalimbali ikiwemo mtu kuprwa fedha akitokea benki na hawakamatwi wahalifu lakini saa hivi Jeshi halina budi kupongezwa kwa operesheni Kali inayofanyika kila siku chini ya Kamanda SAP Jumanne Muliro

 

Pamoja na hayo amewataka Wazazi, Walezi kuwa karibu na Watoto katika siku hiyo ya Sikukuu kwani kunakuwa na kupotea kwa watoto na kuwasihi wasiwaruhusu kwenda kwenye kumbi za starehe wakiwa wenyewe.

 

Previous articleWAHAMIAJI HARAMU WATAFUNA BIL.3.7/- MAGEREZANI _ MAGAZETINI LEO IJUMAA APRILI 07/2023
Next articleUJENZI WA ZAHANATI KWA UFADHILI WA TASAF WAFIKIA ASILIMIA 95

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here