Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Angellah Kairuki amekabidhi magari 43 kwa Watendaji wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Makatibu Tawala Wasaidizi wanaoshughulika na Miuondombinu katika ngazi za Mikoa.
Akizungumza Katika hafla yakukabidhi magari hayo Julai 5 , 2023 Katika Makao Makuu ya TARURA Mtumba Jijini Dodoma Kairuki amesema magari hayo ni kwaajili ya watendaji ili kuwawezesha kuboresha utendaji kazi wao.
Waziri Kairuki amesema magari 30 kati ya 43 ni kwa ajili ya matumizi ya Ofisi za Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) makao makuu na mikoa na magari 13 ni kwa ajili ya ofisi za wakuu wa mikoa kwa ajili ya usimamizi wa kazi za miundombinu.