Home KITAIFA KAIMU MENEJA WA TANROADS TABORA: MRADI WA BARABARA YA KAZILAMBWA-CHAGU KWA KIWANGO...

KAIMU MENEJA WA TANROADS TABORA: MRADI WA BARABARA YA KAZILAMBWA-CHAGU KWA KIWANGO CHA LAMI KUWEZESHA USAFIRI NA USAFIRISHAJI KATI YA TANZANIA NA NCHI JIRANI

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora, Mhandisi Rwegoshora Michael akielezea mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilamwa-Chagu (KM 36) kipande cha kilometa 26 ambazo zipo ndani ya Mkoa wa Tabora Aprili 19, 2023

 

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora, Mhandisi Rwegoshora Michael akielezea mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu (KM 36) kipande cha kilometa 26 ambazo zipo ndani ya Mkoa wa Tabora Aprili 19, 2023
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Ngoko Mirumbe akielezea mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu (KM 36) kipande cha kilometa 10 ambazo zipo ndani ya Mkoa wa Kigoma Aprili 19, 2023

Na Mwandishi Wetu, Tabora

Kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kazilambwa hadi Chagu yenye urefu wa kilometa 36 kunatajwa kuwezesha shughuli mbalimbali za usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria kati ya nchi ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Rwanda na hatimaye kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Faida hiyo muhimu kiuchumi inatokana na kwamba ujenzi wa barabara hiyo utatuunganisha Mkoa wa Kigoma na Tabora huku ikitatua changamoto ya muda mrefu ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma na mikoa mingine nchini na hivyo kuwezesha kufika kwa urahisi katika nchi hizo.

Hayo yamesemwa Aprili 19, 2023 na Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tabora, Mhandisi Rwegoshora Michael wakati wa kutembelea mradi huo kuona maendeleo ya utekelezaji ambapo amesema, hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 89.62.

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora, Mhandisi Rwegoshora Michael akielezea mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu (KM 36) kipande cha kilometa 26 ambazo zipo ndani ya Mkoa wa Tabora Aprili 19, 2023

Mhandisi Rwegoshora ameendelea kwa kusema kuwa, mradi unaotekelezwa na mkandarsi STECOL Corporation chini ya mhandisi mshauri TANROADS Engineering Consulting Unit (TECU) ambapo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali yake ikiwemo kutoa fedha za utekelezaji wa miradi pamoja na kuwalipa wakandarasi wanaotekeleza miradi ikiwemo miradi ya ujenzi barabara kwa wakati.

“TANROADS Mkoa wa Tabora tunaishukuru na kupongeza serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa inazozifanya ili kukamilisha malipo ya wakandarasi ikiwemo mkandarsi wa mradi huu, mkandarsi wa mradi huu (STECOL) analipwa kwa wakati” alisema mhandisi Rwegoshora

Kikuta shoto (keep left) ambacho ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu kwa kiwango cha lami ujenzi wake ukiwa unaendelea

Akiongea katika ziara hiyo, Mhandisi Mshauri kutoka TANROADS Engineering Consulting Unit, Mhandisi Isaya Mosha ameeleza kuwa, barabara ya Kazilambwa-Chagu ina urefu wa kilometa 36 ambapo kilometa 26 ziko katika Mkoa wa Tabora na kilometa 10 ziko katika Mkoa wa Kigoma na kuongeza kuwa, kama mhandisi mshauri anapata furaha kuona wanaelekea kukamilisha mradi huo.

Vilevile Mhandisi Mosha amesema, kama mkandarsi mshauri wataendelea kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara hiyo kwa kujiridhisha viwango stahiki kulingana na vigezo vya muda na mkataba.

“Tunajiridhisha kwa kiwango kinachostahili kutokana na mkataba, kwamba kazi inafanyika kwa kiwango kinachostahili” alisema Mhandisi Mosha na kuongeza kuwa

“Manufaa ya mradi huu ni pamoja na kutoa fursa za ajira kwa zaidi ya watu 400, kuchimba visima vitano na kuboresha baadhi ya barabara za michepuko kutoka katika barabara kuu zinazoelekea katika maeneo yanayopatikana huduma mbalimbali za kijamii”

Kambi ya mkandarasi STECOL Cooperation anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu (KM 36) kwa kiwango cha lami iliyopo kijiji cha Ugansa wilayani Kaliua mkoani Tabora

Akiongelea utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa Mkoa wa Kigoma, Kaimu Meneja wa TANROADS wa mkoa huo, Mhandisi Ngoko Mirumbe amesema, kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo utatoa fursa kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma kwenda mikoa ya jirani ikiwemo Tabora au kwenda mikoa ya mbali ikiwemo Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya shughuli za biashara

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Ngoko Mirumbe akielezea mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu (KM 36) kipande cha kilometa 10 ambazo zipo ndani ya Mkoa wa Kigoma Aprili 19, 2023

“Kukamilika kwa barabara hii ni fursa kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma kufika kwa wakati katika mikoa ya Tabora, Dar es Salaam na mikoa mingine nchini” alisema Mhandisi Mirumbe

Akielezea hali ilivyokuwa hapo zamani, Mhandisi Mirumbe amebainisha kuwa, awali watu wa Mkoa wa Kigoma walikuwa wakisafiri kuelekea Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Nyakanazi lakini sasa wanasafiri kupitia ya Tabora ambapo zaidi ya kilometa 300 zimepungua na hivyo kupunguza gharama za usafiri na kuokoa wakati ambao ulikuwa ukipotea barabarani wakitumia njia ya Nyakanazi.

Kazi mbalimbali za ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu KM 36 kwa kiwango cha lami zikiwa zinaendelea kama zilivyokutwa na mpiga picha wetu hapo jana Aprili 19 ,2023

Wakiongea kwa nyakati tofauti, wananchi wa kijiji cha Ugansa wilayani Kaliua, Anastazia Robert, Mohammed Seleman, Adide Matongo na Arasul Maftaha wameeleza changamoto mbalimbali walizokuwa wakikumbana nazo kabla ya ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo barabara hiyo kutopitika nyakati za mvua, changamoto ya kupata usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ambapo sasa changamoto hizo zikigeuka historia ambapo hawakusita kutoa shukrani kwa serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujio wa mradi huo uliochochea ukuaji wa uchumi na kuibua fursa za kiuchumi ikiwemo biashara maeneo ambayo barabara hiyo inapita.

Mwananchi Adide Matongo, mkazi wa kijiji cha Ugansa wilayani Kaliua akiongelea maendeleo na fursa mbalimbali zilizoibuliwa kupitia ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu kwa kiwango cha lami Aprili 19, 2023
Mwananchi Mohamed Seleman, mkazi wa kijiji cha Ugansa wilayani Kaliua akiongelea maendeleo na fursa mbalimbali zilizoibuliwa kupitia ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu kwa kiwango cha lami Aprili 19, 2023

 

Miradi ya ujenzi wa barabara yenye jumla ya kilometa 238. 9 kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 321 imetekelezwa mkoani Tabora. Kati ya miradi hiyo ni mradi mmoja ndio bado unaendelea kutekelezwa na umefikia asilimia 89.62 ambao ni mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Kazilambwa-Chagu (KM 36), jambo ambalo linatajwa kuwa ni hatua na maendeleo makubwa katika ngazi ya mkoa

Previous articleMRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MARAGARASI-ILUNDE-UVINZA KWA KIWANGO CHA LAMI KUKAMILIKA OKTOBA, 2023
Next articleWATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA KUVUTA MOSHI WA JENERETA DAR ES SALAAM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here